Maria De Mattias Secondary School - Items filtered by date: أيلول/سبتمبر 2024
السبت, 21 أيلول/سبتمبر 2024 07:41

USAILI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2024/2025

NAFASI ZA PRE-FORM ONE KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025

Uongozi wa Shule ya Sekondari Maria De Mattias inayopatikana Kisasa “B” Manispaa ya Dodoma, unawatangazia wazazi/walezi wote nafasi za masomo ya PRE-FORM ONE na FORM ONE kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

FOMU ZA KUJIUNGA

Fomu za kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025 zinapatikana maeneo yafuatayo kwa gharama ya Tsh. 20,000/= tu.

  • Shuleni Maria De Mattias (Dodoma).
  • Katika tovuti yetu ya shule ambayo ni www.mariademattiassec.sc.tz.
  • Morogoro, kwa Masista Waabuduo Damu ya Kristo (Kola B): 0762987474
  • Dar es Salaam, Mbezi Beach-Tangi Bovu kwa Masista: 0628291000
  • Dar es Salaam, Msimbazi Center Chumba namba 22. 0715265446
  • Moshi Bookshop (Kilimanjaro).

NAMNA YA KUJIUNGA

Usaili (interview) utafanyika tar 30/09/2024 shuleni Maria De Mattias (Dodoma) na Mbezi Beach Tangi Bovu (Dar es Salaam).

Muda wa kuripoti kituo cha mtihani ni saa moja kamili asubuhi.

NB: Shule ya Sekondari Maria De Mattias ni shule ya Bweni kwa O-LEVEL na A-LEVEL na ni ya wasichana tu.

“Mlete mwanao Maria De Mattias Sekondari kwa Elimu na Malezi bora”.

Published in News

Contact us

Web Traffic

Today54
Yesterday1326
This week2264
This month1380
Total201961

Follow us on

Top